Wahusika

Jay Godsall, Mkurugenzi mkuu

Jay Godsall ndiye mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Solar Ship. Amekuwa kiongozi wa kampuni hii tangu ianzilishwe kwenye mwaka wa 2006. Kabla ya hapo, alikuwa kati ya waanzilishi wa kampuni ya Fio inayoshughulika na kuorodhesha magonjwa ya mimea. Alihusika na kuajiri wasimamizi wa kwanza na pia katika kukusanya fedha za uwekezaji zilizotimia dola milioni ishirini na tano. Utaalamu wake ni kuanzilisha kampuni za teknolojia. Yeye pia ni mtaalamu wa mbinu za kuokoa fedha, wakati na hatari katika kampuni na ametambulika huko Canada na duniani kote. 

John Hutchinson, Afisa mkuu wa kiufundi

John Hutchison ana ujuzi wa miaka thelathini katika ujenzi na ukarabati wa ndege na ni mwanzilishi wa mifumo ya kawi ya kutumika kwenye sehemu za mashambani. John pia ni rubani wa ndege za kawaida na zile za helikopta. Anatambulika duniani kama mtaalamu wa aina yake katika ujenzi wa betri za kutumika kwenye sehemu za mashambani. Alisimamia uhandisi wote, uchoraji na ujenzi alipokuwa mkuu wa teknolojia katika kampuni ya Free Play Energy iliyoodhoreshwa kwenye soko la hisa la London. John ana shahada ya uhandisi, ya sheria na shahada ya juu ya utawala wa biashara kutoka kwenye chuo kikuu cha Cape Town.   

Michel Rugema, Afisa mkuu wa uendeshaji

Michel Rugema ana ujuzi wa miaka ishirini kama mkuu wa uendeshaji kwenye sehemu za mashambani. Amekuwa mkurugenzi wa kampuni na mashirika mengi zikiwemo USAID barani Africa na Haiti na mahoteli ya kifahari mjini New York. Alikuwa mwanzilishi na mkurugenzi wa kampuni ya Archipel huko Burundi inayohusika na biashara ya mikahawa. Amehitimu na shahada ya Masters katika ukurugenzi kutoka kwenye chuo kikuu cha Cornell alipokuwa pia mkuu wa uendeshaji. Shahada yake ya kwanza ni ya kutoka Chuo kikuu cha Montréal. 

Dr. Sébastién Fournier, Mkuu wa uvumbuzi

Daktari Fournier hushughulika na shughuli zote za uvumbuzi katika kampuni ya Solar Ship na pia huhusika na mbinu za kupunguza hatari zinazoweza kusababisha kuvujwa kwa fedha katika kampuni. Kabla ya kujiunga na Solar Ship, Daktari Fournier alihusika na shughuli za uvumbuzi katika kampuni ya Fio. Alizindua mbinu ya kwanza ulimwenguni ya kuorodhesha magonjwa ya mimea. Alipata shahada yake katika kemia kutoka kwenye chuo kikuu cha Toronto.