AINA ZA NDEGE

Solarship imejengwa kwa kuhusisha aina za kisasa za teknologia na nyenzo imara lakini nyepesi, betri nyepesi na vyuma bora vya kuzalisha nishati kutokana na miale ya jua. Kwa kutumia aina yake ya nguvu, ndege hii ina uwezo wa kubeba uzito sawa na trela kwa urahisi zaidi ya ndege za kawaida. Muundo wake pia unawezesha ongezeko la uzito kadri ya ukubwa wa ndege. 

Solar Ship inajenga aina tatu ya ndege, Caracal, Chui na Nanuq kulingana na matakwa mbali mbali ya wateja.

Caracal

Ndege yetu ndogo zaidi ni ile ya Caracal inayosifika kwa mbio na ufanisi kama duma wa Africa. Ndege hii inaweza tumika katika kazi zote, zikiwemo za upepelezi wa angani. Ndege hii ina uwezo wa kupaa na kutua katika sehemu ndogo, inaweza paa safari ndefu kwa kutumia kiasi kidogo cha mafuta na hubeba mizigo au abiria kulingana na matakwa mbali mbali.  

Chui

Ndege hii imepewa jina la chui kwa sababu ya mwendo wake wa kasi, utulivu na nguvu na inaweza linganishwa na trela ndogo zinazotumika kubeba mizigo. Ni kubwa zaidi ya Caracal na imejengwa na njia za kisasa ili kupaa na kutua kwa utulivu. Ndege hii inasifika kwa ufanisi katika utumizi wa mafuta. Hupaa kwa safari ndefu zaidi na pia hutumia nishati ya miale ya jua.

Nanuq

Ndege hii imetoa jina lake kwenye kakadubu, mnyama anayepatikana kwenye nchi za baridi barani uropa. Ndege hii inasifika kwa nguvu zake na inaweza kulinganishwa na trela za magurudumu kumi na nane. Kazi hasa ya ndege hii ni kubeba mizigo na imetengezwa na ufanisi mkubwa ili kutumia mafuta kidogo na kutua katika sehemu zisizo na barabara. Ndege hii pia ina uwezo wa kupaa kwa masafa marefu zaidi kwa kutumia nishati ya miale ya jua.  

Wafadhili wetu

Zenair_logo_web

SolidWorks_logo_web

Cad_Microsolutions_web

rotec_logo_web